Zaidi ya watu 75 wapoteza maisha katika mlipuko Ufaransa, Rais Hollande atangaza hali ya hatari

304
0
Share:

Wakati Wafaransa wakiwa katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Bastille, umetokea mlipuko katika mji wa Nice kutoka katika lori na kusababisha vifo vya wanaokadiliwa kufikia 80 na wengine wakipata majeruhi kutokana na mlipuko huo

Taarifa kutoka Ufaransa zinaeleza kuwa lori hilo lilifika katika eneo ambalo lina watu wengi na kutokea mlipuko kisha baadae kulipatikana bunduki na vifaa vingine vya ulipuaji katika lori hilo.

Licha ya watu wanaokadiliwa kupoteza maisha kutajwa kufikia 80, lakini pia idadi ya majeruhi ambao wamepatikana katika tukio hilo wanatajwa kuwa kufika 50.

Meya wa mji wa Nice, Christian Estrosi amesema kuwa dereva wa lori hilo alipeleka gari katika eneo ambalo lilikuwa na watu wengi kisha kutokea mlipuko umeopelekea kutokea kwa vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.

Kutokana na tukio hilo, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza hali ya hatari kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuimarisha hali ya usalama na kusema kuwa Wafaransa kwa sasa wapo katika vita na makundi ya kiislam ambayo yamekuwa yakiwashambulia..

Hii inakuwa sio mara ya kwanza kutokea kwa shambulio nchini Ufaransa kwani mwaka jana mwezi Novemba kulitoke shambulio lingine lililosababisha vifo vya watu 130.

Share:

Leave a reply