Zantel yadhamini tamasha la Wanachuo la ‘CHEM CHEM BONFIRE’ dar

402
0
Share:

Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel imeweza kudhamini tamasha maalum kwa wanachuo lilopewa jina la ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ ambalo lilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali waliweza kutoa burudani kali nay a aina yake wakiwemo wasanii nguli Mkongwe Juma Nature, Young Killer na wengine wengi ambao walipagawisha wanafunzi hao wa vyuo waliojitokeza kwa wingi kwenye ukumbi huo wa New  Msasani  Club.

Juma Nature, Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Juma Kassim Nature akiwapagawisha Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu  vya  jiji la Dar es Salaam katika Tamasha lililoratibiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel lilopewa jina la ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ ambalo lilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Happy & Ibra, Wasanii wa kizazi kipya wanaochipukia, Ibrahim Jakob na Happy Best wakishambulia jukwaa kwenye Tamasha la wanachuo lijulikanalo kama ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ lililofanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

 

Young Killer, Msanii wa Muziki wa Bongo Flaver, Young Killer akiimba pamoja na Wanafunzi wa Vyuo vikuu  vya  jiji la Dar es Salaam kwenye Tamasha lililoratibiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel lililopewa jina la ‘Zantel Chem Chem Bonfire’ ambalo lilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Club hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply