ZANTEL YATOA MSAADA WA MIAMVULI 60 KWA CHUO CHA USTAWI WA JAMII DAR

164
0
Share:

Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa kuthamini elimu sekta ya elimu,  imeweza kutoa miamvuli 60, kwa Chuo cha Ustawi wa Jamii hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Miamvuli hiyo 60 ilitolewa kwa chuo hicho kwa lengo la kuwakinga jua wanafunzi wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo. Kwa upande wake  Rais wa Wanafunzi chuo cha Ustawi, John Filimon aliishukuru Zantel kwa msaada huo kwani itawasaidia kujikinga na mvua wakati wa jua kali na hata wakati wa mvua kwani walikuwa wakipata taabu hapo awali.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu (kushoto) akisimika moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa  Chuo cha Ustawi wa Jamii hivi karibuni jijini Dar es salaam.Jumla ya Miamvuli 60 ilitolewa kwa chuo hicho kwa lengo la kuwakinga jua wanafunzi wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo. Katikati ni Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Remidius Leonard na kulia ni Rais wa Wanafunzi, John Filimon.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo eneo la Bamaga jijini Dar es salaam wakijisomea kwenye moja ya kizimba kilichosimikwa moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel hivi karibuni jijini Dar es salaam. Jumla ya miamvuli 60 ilitolewa kwa ajili ya kuwakinga jua Wanafunzi wa chuo hicho wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo.

Muonekano mpya na wa kuvutia baada ya kuwekwa kwa miamvuli hiyo ya Zantel chuoni hapo

Leave a reply