Zitto Kabwe amtembelea Mbwana Samatta nyumbani kwake Ubelgiji

192
0
Share:

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe jana alimtembelea Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta kwa ajili ya kumjulia hali.

Zitto amebainisha hilo leo kupitia taarifa yake kwa umma, ambapo amesema anamuomba Mungu amuwezeshe katika kutimiza ndoto zake.

“Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji, Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta,” amesema na kuongeza.

“Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi.”

Share:

Leave a reply